WABUNGE nchini Uganda wanatarajia kutoa asilimia moja ya mishahara yao ya mwezi huu ili kuisaidia timu ya taifa ya nchi hiyo The Cranes katika michuano ya Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii Gabon. Spika wa bunge hilo, Rebecca Kadaga amesema wamekubaliana kuchanga dola 150 kwa kila mbunge na anatarajia kwenda nchini Gabon na fedha hizo. Jumla ya kiasi kitakachokusanywa na wabunge ni dola 58,451. Serikali ya Uganda imetoa kiasi cha dola 540,716 ikiwa ni pungufu ya kiasi cha dola milioni mbili walichoataka Shirikisho la Soka la nchi hiyo-FUFA. Kwasasa The Cranes wameweka kambi yao katika Falme za Kiarabu.
No comments:
Post a Comment