Wednesday, January 11, 2017

RONALDO ATAJWA TUZO NYINGINE.

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametajwa katika orodha ya watakaogombea tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka ya Laureus. Nyota huyo amekuwa na miezi 12 yenye mafanikio baada ya kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Euro 2016. Kiwango kikubwa alichoonyesha kimemfanya kutwaa tuzo za Ballon d’Or na tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA. Tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka hupigiwa kura na wanahabari na Ronaldo atakuwa akishindana na nyota wengine wakiwemo nyota wa mpira wa kikapu Marekani Steph Curry na Lebrone. Pia watakuwepo mwanariadha nyota wa mbio fupi wa Jamaica Usain Bolt, mwanaridha nyota wa Uingereza Sir Mo Farah na kinara wa mchezo wa tenisi duniani Sir Andy Murray. Kama akitwaa tuzo hiyo Ronaldo atakuwa mchezaji soka wa kwanza kufanya hivyo toka kuanzishwa kwa tuzo hizo mwaka 2000. Mshindi wa tuzo hiyo anatarajiwa kutangazwa Februari 14 mwaka huu jijini Monaco.

No comments:

Post a Comment