MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amekingia kifua uamuzi wa kikosi alichokichagua kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la FA waliotoka sare ya bila kufungana na klabu ya daraja la pili ya Plymouth. Liverpool sasa wanakabiliwa na safari ya kwenda Devon kwa ajili ya mchezo mwingine wa marudiano huku wakikabiliwa na mechi sita mwezi huu. Klabu hiyo pia inakabiliwa na mchezo wa mikondo miwili wa nusu fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Southampton pamoja na mechi za Ligi Kuu dhidi ya Manchester United, Swansea City na Chelsea. Hata hivyo alipohojiwa kuhusiana na kikosi alichotumia, Klopp amesema hadhani kama alifanya makosa kuchagu kikosi hicho.
No comments:
Post a Comment