MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho ameunga mkono mapendekezo ya kuongeza timu kufikia 48 katika Kombe la Dunia akiamini kuwa wachezaji watalindwa vyema. Rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Gianni Infantino ana matumaini mpango wake kuwa na makundi 16 yenye timu tatu kuanzia michuano ya mwaka 2026 utapitishwa wakati wa kikao cha kamati ya utendaji ya shirikisho hilo wiki ijayo. Muungano wa Vilabu Ulaya ambao United pia ni mjumbe wake, tayari wameshaonyesha kutounga mkono pendekezo hilo lakini Mourinho yeye anaunga mkono. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo, Mourinho amesema anaunga mkono kwasababu ana uhakika FIFA itazingatia maslahi ya wachezaji kwa kutowachezesha mechi nyingi zaidi kuliko sasa.
No comments:
Post a Comment