SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA kesho linatarajiwa kupigia mpango wa kuongeza timu katika michuano ya Kombe la Dunia kufikia 48 kuanzia mwaka 2026. Mpango huo wa kuongeza timu umependekezwa na rais wa shirikisho hilo Gianni Infantino. Infantino raia wa Uswisi, ambaye amedai mpango wake huo unaungwa mkono kwa kiasi kikubwa, anataka kuwe na makundi sita yatakayokuwa na nchi tatu huku zile mbili za juu zikisonga mbele kwenye hatua ya mtoano. Kama mapendekezo hayo yakipitishwa, michuano hiyo itakuwa imepanuliwa kwa mara ya kwanza toka mwaka 1998 ambapo waliongeza timu kutoka 24 mpaka 32.
No comments:
Post a Comment