MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwenye sherehe zilizofanyika jijini Zurich jana usiku. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 ametwaa tuzo hiyo akiwashinda nyota wa Barcelona Lionel Messi na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid. Ronaldo pia alitwaa tuzo ya Ballon d’Or Desemba mwaka jana ambapo tuzo zote hizo amezipata kutokana na mafanikio aliyopata katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Madrid na Euro 2016 akiwa na Ureno. Mwanadada Carli Lloyd wa Marekani aliteuliwa mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wanawake.
Meneja wa Leicester City Claudio Ranieri amechaguliwa kocha bora wa mwaka, kocha wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake ya Ujerumani Silvia Neid ameshinda tuzo hiyo kwa upande wa wanawake na Mohd Faiz Subri wa klabu ya Penang ya Malaysia ameshinda tuzo ya Puskas ya bao bora la mwaka.
No comments:
Post a Comment