Tuesday, January 10, 2017

MENEJA WA BARCELONA ADAI ULIKUWA UAMUZI WA WACHEZAJI KUTOHUDHURIA TUZO ZA FIFA.

MENEJA wa Barcelona, Luis Enrique amesema uamuzi wa kutohudhuria sherehe za utoaji tuzo za FIFA uliamuliwa na wachezaji wenyewe. Nyota wa timu hiyo akiwemo Lionel Messi, Luis Suarez, Neymar, Gerard Pique na Andres Iniesta hawakusafiri kwenda jijini Zurich kwenye tukio hilo jana, huku klabu ikithibitisha kuwa kikosi chao kialiamua kubakia ili kuendelea na maandalizi yao ya mchezo wa Kombe la Mfalme dhidi ya Athletic Bilbao Alhamisi hii. Cristiano Ronaldo alimshinda Messi katika tuzo hizo na kudai kuwa angependelea zaidi nyota huyo wa Barcelona angekuwepo kwenye tuzo hizo wakati Roberto Carlos na Dani Alves pia wakiponda uamuzi huo wa kutohudhuria. Akihojiwa Enrique amesema ulikuwa ni uamuzi wa wachezaji kuamua kama wanataka kwenda au la lakini akasisitiza kuunga mkono chaguo lao la kubakia kwa umuhimu wa mchezo wao dhidi ya Bilbao.

No comments:

Post a Comment