NYOTA WA MADRID WAIPONDA BARCELONA KUTOHUDHURIA TUZO ZA FIFA.
NYOTA wa Real Madrid, Luka Modric, Sergio Ramos na Cristiano Ronaldo wote wameeleza kusikitishwa kwao kwa wachezaji wa Barcelona kutohudhuria sherehe za utoaji tuzo za Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Madrid ndio waliotawala zaidi tuzo hizo kufuatia Ronaldo kuwa mchezaji bora wa mwaka duniani akimshinda Lionel Messi huku klabu hiyo ikitoa wachezaji watano katika kikosi bora cha mwaka akiwemo Ramos. Barcelona pia wana wachezaji wanne walioteuliwa katika kikosi hicho lakini bado hakuna mchezaji yeyote wa timu hiyo aliyehudhuria sherehe hizo zilizofanyika jijini Zurich. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo, Modric amesema kwa mawazo yake anadhani Barcelona walipaswa kuhudhuria sherehe hizo. Naye Ronaldo alieleza kusikitishwa kwake kwa kukosekana kwa Messi kwenye tuzo huku akiahidi kwamba kama akiendelea kuchagulia katika tuzo zijazo atahakikisha anakuwepo.
No comments:
Post a Comment