KIUNGO John Mikel Obi ametangaza kuondoka Chelsea rasmi na kwenda kujiunga na klabu ya Tianjin TEDA inayoshiriki Ligi Kuu ya China. Nyota huyo wa kimataifa wa Nigeria mwenye umri wa miaka 29, ameichezea Chelsea mechi 372 toka ajiunge nao mwaka 2006. Katika barua yake kwenda kwa mashabiki, Obi Mikel amesema imekuwa ni heshima kubwa kwake kuichezea klabu hiyo lakini anadhani wakati umefika wa kwenda kutafuta changamoto nyingine. Obi Mikel amefanikiwa kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu, manne ya Kombe la FA moja na Europa League na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Obi Mikel anakuwa mchezaji wa pili wa Chelsea kutimkia China katika wiki za karibuni baada ya Oscar aliyehamia Shanghai SIPG.
No comments:
Post a Comment