Friday, January 6, 2017

PIQUE ALIA NA WAAMUZI BAADA YA KIPIGO.

BEKI wa Barcelona, Gerard Pique amedai kuwa waamuzi nchini Hispania wanaipendelea Real Madrid baada ya klabu hiyo kuchapwa mabao 2-1 na Athletico Bilbao katika mchezo wa Kombe la Mfalme uliochezwa jana usiku. Barcelona walilalamikia penati mbili moja iliyomhusisha Neymar na nyingine Pique, ambazo zilikataliwa katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza hatua ya timu 16 bora, ingawa baadae wenyeji Bilbao walipoteza wachezaji wawili kwa kadi nyekundu Raul Garcia na Ander Iturraspe. Akihojiwa Pique amesema penati hizo zilikuwa za wazi kabisa lakini anadhani wanajua kwanini wanafanyiwa hivyo. Pique aliendelea kudai kuwa waamuzi wamekuwa wakiwakwamisha kwa kuonyesha upendeleo kwa Madrid akitolea mfano wa mechi yao ya jana dhidi ya Sevilla ambayo walishinda mabao 3-0.

No comments:

Post a Comment