RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika-CAF, Issa Hayatou ameitwa na waendesha mashitaka nchini Misri kwa uchunguzi kufuatia tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi yake. Mojawapo ya tuhuma zinazomkabili ni ile ya kutoa haki za matangazo kwa michuano mbalimbali ya soka Afrika kwa kampuni ya inayojihusisha na masuala ya habari ya Legardere Sports. Kwa mujibu ya Mamlaka zinazosimamia mashingano mbalimbali nchini Misri, Hayatou anatuhumiwa kwa kutoweka wazi tenda za mashinano hayo kama inavyotakiwa na sheria za nchi hiyo. CAF makao yake makuu yako jijini Cairo, hivyo shughuli zake zozote inabidi zifuate sheria za hapo. Hayatou mwenye umri wa miaka 70, alichaguliwa mwaka 1998 na kwasasa anatumikia muhula wake saba.
No comments:
Post a Comment