Monday, January 2, 2017

WENGER ALISIFIA BAO LA GIROUD.


MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa bao murua la Olivier Giroud alilofunga katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Crystal Palace ni moja kati ya mabao yake tano bora aliyopata kushuhudia katika kipindi cha miaka 21 akiwa na klabu hiyo.
Mabao ya kina Thierry Henry na Dennis Bergkamp nayo yapo katika orodha yake lakini amesema bao hilo la jana milele litakuwa la Giroud pekee.
Wenger amesema kiufundi sio jambo lisilowezekana lakini unatakiwa na uwezo tofauti kwani mpira wa krosi haukuja kama ilivyotakiwa na Giroud alifanya jambo la kipekee.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amesema ilikuwa kama bahati kwani mpira haukuja kama ilivyotakiwa.

No comments:

Post a Comment