Wednesday, January 4, 2017

CHAPECOENSE KUSAJILI 20 WAPYA KWA AJILI YA MSIMU MPYA.

MKURUGENZI wa michezo wa Chapecoense, Rui Costa amedai kuwa klabu hiyo inatarajia kusaini wachezaji wapya 20 kwa ajili ya msimu mpya huku fulana mbili za wachezaji walionusurika katika ajali zikituzwa bila kwa matumaini kuwa wanaweza kurejea uwanjani tena. Klabu hiyo ilipoteza karibu wachezaji wote waliofariki katika ajali ya ndege nchini Colombia Novemba 28 mwaka huu. Klabu hiyo ndogo inayotoka kusini wa Brazil ilikuwa njiani kuelekea Medelin kucheza na Atletico Nacional katika mchezo wa fainali ya Copa Sudamericana kabla ya kupata ajali hiyo milimani na kuua watu 71. Mabeki Neto na Alan Ruschel walisalimika katika ajali hiyo sambamba na kipa wa akiba Jackson Follmann ambaye mguu wake umekatwa kutokana na ajali hiyo. Costa amesema wachezaji wote watatu waliopona ajalini bado wana nafasi ya kucheza na hakuna mchezaji yeyote atakayevaa jezi zao na pamoja na kwamba Follmann hataweza lakini anaweza kushiriki kwa upande mwingine. Costa aliendelea kudai kuwa klabu hiyo itasajili wachezaji 18 mpaka 20 wapya kabla ya kuanza kwa msimu Januari 26 kwa mchezo wa nyumbani dhidi ya Joinville.

No comments:

Post a Comment