Friday, February 3, 2017

AFCON 2015: GRANT AKISIFU KIKOSI CHAKE PAMOJA NA KUTOLEWA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ghana, Avram Grant amesisitiza kuwa imekuwa michuano mizuri kwa timu hiyo pamoja na kutolewa katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika na Cameroon jana. Hiyo inakuwa mara ya sita kwa Ghana kucheza nusu fainali ya michuano hiyo lakini walijikuta wakipoteza kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Michael Ngadeu na Christian Bassogog huko Franceville. Ghana imeendelea na ukame wa mataji baada ya mara ya mwisho kutwaa taji hilo mwaka 1982. Akizungumza na wanahabari Grant amesema pamoja na kutolewa lakini anaona wamepata mafanikio kwani walikuwa bora katika mchezo huo. Grant aliendelea kudai kuwa mchanganyiko mzuri wa kikosi cha Ghana ana uhakika wanaweza kupata mafanikio makubwa huko mbele.

No comments:

Post a Comment