Friday, February 3, 2017

WAKALA WA AGUERO AIZODOA MADRID.

WAKALA wa Sergio Aguero amepuuza tetesi zinazomhusisha mshambuliaji huyo wa Manchester City kuhamia Real Madrid majira ya kiangazi akisisitiza kuwa hatakwenda popote. Maswali kuhusu mustakabali wa Aguero yalizuka baada ya meneja Pep Guardiola kumuacha katika benchi na badala yake kumtumia Gabriel Jesus katika ushindi wa mabao 4-0 waliopata dhidi ya West Ham United. Aguero ambaye amefunga mabao 11 katika mechi 17 za Ligi Kuu alizocheza msimu huu, pia aliwekwa katika benchi katika mchezo City waliofungw amabao 4-0 na Barcelona Octoba mwaka jana na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Burnley mwezi uliopita. Kufuatia hali hiyo tetesi zikazuka kuwa Madrid wanapanga kumuwania majira ya kiangazi huku Juventus, Paris Saint-Germain na Atletico Madrid nazo zikitajwa kumfuatilia. Hata hivyo, wakala wake Hernan Reguera alikanusha taarifa hizo na kudai mteja wake anafurahia maisha katika klabu hiyo na hana mpango wa kwenda popote.

No comments:

Post a Comment