Friday, February 3, 2017

BERAHINO AZUA MJADALA STOKE.

MENEJA wa Stoke City, Mark Hughes amesema Saido Berahino alikuwa ameshatumikia adhabu ya kutocheza kwa wiki sita kabla ya kuondoka West Bromwich Albion. Kauli ya kocha huyo imekuja kufuatia taarifa iliyotolewa katika magazeti kuwa mshambuliaji huyo alifungiwa baada ya kushindwa vipimo vya dawa za kusisimua misuli. Hughes amesema nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye alijiunga na Stoke kwa kitita cha paundi milioni 12 Januari mwaka huu, amefungiwa kutokana na matatizo ya kinidhamu na Shirikisho la Soka la Uingereza-FA. Hughes mwenye umri wa miaka 53 aliendelea kudai kuwa haoni sababu ya kutomtumia Berahino katika mchezo wao wa ligi Jumamosi hii.

No comments:

Post a Comment