Friday, February 3, 2017

WENGER AMUHOFIA KANTE KESHO.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini N’Golo Kante, mchezaji ambaye alijaribu kumsajili, ni mtu muhimu kwa Chelsea katika mbio za Ligi Kuu. Arsenal watasafiri kwenda Stamford Bridge Jumamosi hii wakiwa wanashika nafasi ya tatu nyuma ya Tottenham Hotspurs kwa tofauti ya mabao na alama 10 nyuma ya vinara Chelsea kufuatia kufungwa mabao 2-1 na Watford Jumanne iliyopita. Chelsea walitoka sare ya bao 1-1 na Liverpool siku hiyo hiyo na Wenger anaamini nafasi waliyopo Chelsea hivi sasa inachangiwa kwa kiasi kikubwa na kazi kubwa inayofanywa na Kante katika nafasi ya katikati. Wenger amesema alitizama mchezo dhidi ya Liverpool na Kante alionekana kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo hivyo sio ajabu kuona Chelsea wapo nafasi hiyo kama walivyokuwa Leicester City mwaka jana. Kwa upande kikosi cha Arsenal, bado kinakabiliwa na matatizo katika nafasi ya kiungo kufuatia kuumia kwa Aaron Ramsey na Santi Cazorla na pia kukosekana kwa Granit Xhaka ambaye anatumikia adhabu.

No comments:

Post a Comment