Monday, February 6, 2017

CAMEROON USO KWA USO NA MABINGWA WA DUNIA.

MABINGWA wapya Cameroon imekuwa timu ya mwisho kufuzu michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuichapa Misri mabao 2-1 katika hatua ya fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika. Mabao yaliyofungwa na Nicolas Nkoulou na Vincent Aboubakar katika kipindi cha pili yalitosha kuwapata taji hilo la tano kwao, pamoja na Mohamed Elneny kuwapa Misri bao la kuongoza. Cameroon inatarajiwa kupambana na mabingwa wa dunia Ujerumani, Chile na Australia katika kundi B kwenye mzunguko wa awali wa michuano hiyo. Cameroon wanaonolewa na Hugo Broos wataanza kampeni zao kwa kucheza dhidi ya mabingwa wa Copa America Chile katika Uwanja wa Spartak jijini Moscow Juni 18 mwaka huu. Siku nne baadae watapambana na Australia huko St. Petersburg kabla ya kukutana na Ujerumani jijini Sochi Juni 25. Cameroon walimaliza kama washindi wa pili katika michuano ya mwaka 2003 ambapo walimpoteza mchezaji wao Marc Vivien Foe aliyefariki uwanjani.

No comments:

Post a Comment