Monday, February 6, 2017

AGUERO HAJUI HATMA YAKE CITY.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero bado anataka kuendelea kubaki katika klabu hiyo lakini atawaachia wenyewe kufanya watakavyotaka mwishoni mwa msimu huu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 aliachwa katika benchi katika mchezo wa pili mfululizo jana. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina aliingia zikiwa zimebaki dakika saba wakati City waliposhinda mabao 2-1 dhidi ya Swansea City. Akizungumza na wanahabari, Aguero amesema miezi hii mitatu iliyobakia anataka kuisaidia klabu na baada ya hapo wataamua kama bado ana nafasi au la.

No comments:

Post a Comment