Thursday, February 2, 2017

DORTMUND YAMCHIMBA "BITI" AUBAMEYANG.

MKURUGENZI wa michezo wa Borussia Dortmund, Michael Zorc amemzuia mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang kutozungumzia suala la kuondoka mwishoni mwa msimu huu katika mahojiano yake siku zijazo. Akizungumza na wanahabari, Zorc amesema walizungumza na Aubameyang kwa kifupi na kumshauri kutojadili mustakabali wake wa baadae katika mahojiano yake na badala yake aelekeze nguvu katika kuisaidia klabu kupata nafasi ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Zorc aliendelea kudai kuwa ana matumaini mazungumzo yake yatakuwa na faida kwani Aubameyang alimulewa. Nyota huyo wa kimataifa wa Gabon ana mkataba na Dortmund unaomalizika mwaka 2020 lakini ameweka wazi anataka kucheza katika klabu ya Real Madrid ili kutimiza ahadi yake aliyotoa kwa babu yake kabla ya hajafa.

No comments:

Post a Comment