Thursday, February 2, 2017

GUARDIOLA ASALIMU AMRI KWA TOURE, AMUITA TENA CHAMPIONS LEAGUE.

KIUNGO wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure ameitwa tena katika kikosi cha Manchester City kwa ajili ya michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kuachwa na meneja Pep Guardiola katika hatua ya makundi. Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Brazil Gabriel Jesus pia ametajwa katika kikosi hicho cha wachezaji 21, kufuatia kuwasili kwake kutoka Palmeiras Januari mwaka huu. Ilkay Gundogan ameachwa katika kikosi hicho kufuatia kiungo huyo wa Ujerumani kutarajiwa kukosa msimu wote uliobakia kutokana na majeruhi ya goti yanayomsumbua. City watakabiliana na Monaco ya Ufaransa katika hatua ya timu 16 bora, na Guardiola tayari alishathibitisha kumjumuisha Toure mwenye umri wa miaka 33 katika kikosi chake mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment