Monday, February 6, 2017

KIPA WA LEICESTER ACHOSHWA NA VIPIGO.

KIPA wa Leicester City, Kasper Schmeichel amesema wanaweza kushuka daraja kama wakiendelea kupoteza mechi zao za Ligi Kuu. Mabingwa hao watetezi wako alama moja juu ya eneo la kushuka daraja kufuatia kipigo cha mabao 3-0 jana dhidi ya Manchester United. Leicester hawajashinda mechi yeyote kwa mwaka huu wa 2017 na hawajafunga bao lolote katika mechi zao tano za ligi zilizopita. Akizungumza na wanahabari, Schmeichel amesema kila mchezaji anaumia kwa hali sio nzuri na jambo muhimu ni kuzinduka na kuhakikisha wanarejesha makali ili kujiokoa kutoshuka daraja.

No comments:

Post a Comment