Source: The Mirror
Klabu ya Manchester City inadaiwa kutaka kumrudia Aymeric Laporte wa Athletic Club majira ya kiangazi pamoja na nyota huyo wa Ufaransa kukaa ofa ya paundi milioni 39 kabla ya kuanza kwa msimu huu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 anaidaiwa kuwekewa kitenzi cha paundi milioni 55 katika mkataba wake na meneja Pep Guardiola anadhani mchezaji huyo ni sahihi kumsajili kuliko Virgil van Dijk wa Southampton ambaye anadaiwa kuwa na thamani ya paundi milioni 50. Laporte ameichezea Athletic mechi 26 msimu huu huku akianza katika mechi 19 za La Liga.
Source: Mirror
Source: Mirror
MENEJA wa Chelsea Antonio Conte anadaiwa kuwindwa kwa udi na uvumba na klabu ya Inter Milan ya Italia. Meneja huyo wa zamani wa Juventus ameibadilisha kwa kiasi kikubwa Chelsea toka atue majira ya kiangazi mwaka jana na kuwafanya kuwa vinara katika msimamo wa Ligi Kuu kwa tofauti ya alama tisa. Wamiliki wa Inter Suning Group anataka kufanya usajili wa nyota kadhaa majira ya kiangazi na wanadhani Conte ndio chaguo sahihi kuirejesha klabu hiyo katika ubora wake wa zamani.
Source: Tuttosport (via ilbianconero).
Source: Tuttosport (via ilbianconero).
KLABU ya Arsenal inadaiwa kutaka kumuwania kiungo Michael Carrick wakati usajili wa majira ya kiangazi baadae mwaka huu. Kiungo huyo anatarajiwa kumaliza mkataba wake Old Trafford mwishoni mwa msimu huu huku Jose Mourinho akionekna kutomuhitaji tena mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35. Meneja wa Arsene Wenger anataka kuimarisha safu yake ya kiungo na Carrick anaonekana kuwa chaguo lake.
Source: The Sun
Source: The Sun
No comments:
Post a Comment