RAIS wa Shirikisho la Soka nchini-TFF, Jamal Malinzi amewataka wadai kujitokeza kuisaidia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys ambao wamefanikiwa kwenda kushiriki michuano ya Mataifa Afrika kwa vijana wa umri huo nchini Gabon Mei mwaka huu. Malinzi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kupata nafasi ya ushiriki kwa vijana hao baada ya timu ya Congo Brazaville kushindwa kumpelekea mchezaji wao Langa ambae alisadikiwa kuwa na umri mkubwa zaidi na kuchezeshwa kwenye mashindano ya vijana. Malinzi amewataka wadau kwa pamoja kusaidiana nao katika kuaindaa timu ya vijana kwani hakika mashindano haya yanahitaji kiasi kikubwa cha fedha takribani dola laki tano (500,000) ili timu iweze kuweka kambi nje ya nchi na hata kupata vifaa vya kutosha na vya kisasa. Malinzi pia aliipongeza serikali kwa msaada wao mkubwa wakati wakipigania haki yao Shirikisho la Soka la Afrika-CAF juu ya mchezaji wa Congo Brazaville aliyezidi umri.
No comments:
Post a Comment