Tuesday, February 7, 2017

INIESTA, BUSQUETS WAREJEA BARCELONA KUONGEZA NGUVU.

BARCELONA imepata ahueni kubwa kuendelea mchezo wao wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Atletico Madrid kufuatia Sergio Busquets na Andres Iniesta kutajwa katika kikosi cha Luis Enrique. Busquets alikosa mechi nne za mwisho za Barcelona kufuatia majeruhi ya goti huku Iniesta akiwa hayupo uwanjani kwa mwezi mmoja kutokana na matatizo ya msuli wa paja. Beki Gerard Pique pia yuko fiti pamoja na kuumia na kutolewa wakati wa mapumziko katika mchezo wa Jumamosi iliyopita dhidi ya Athletic Bilbao, lakini Neymar hatakuwepo kutokana na kutumikia adhabu. Barcelona wanakwenda katika mchezo huo wakiwa mbele ya mabao 2-1 waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa katika Uwanja wa Vicente Calderone.

No comments:

Post a Comment