Tuesday, February 7, 2017

RAIS WA ATLETICO AWAKATAA COSTA NA AGUERO.

RAIS wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo amekanusha tetesi kuwa klabu hiyo inaweza kutuma ofa kwa ajili ya kuwarejesha Diego Costa au Sergio Aguero kama rufani yao ya kufungiwa kusajili itashinda. Aguero ameondolewa katika kikosi cha kwanza na meneja wa Manchester City Pep Guardiola na badal yake kumtumia sana chipukizi wa Brazil Gabriel Jesus katika mechi mbili zilizopita na kuzusha tetesi za mustakabali wake msimu ujao. Pamoja na Aguero kufunga mabao 102 katika kipindi cha maika mitano aliyokaa Atletico kabla ya kujiunga na City mwaka 2011, Cerezo amemponda nyota huyo wa kimataifa wa Argentina kwa kuondoka vibaya. Cerezo amesema kama Aguero angeondoka kawaida na mazingira mazuri kungekuwa hakuna tatizo lakini hajui kitu gani kilimtokea kwani aliondoka vibaya. Kwa upande wa Costa, Cerezo amesema hadhani kama Chelsea watamuacha aondoke hivi karibuni hivyo haoni kama kuna dalili zozote za kumrejesha.

No comments:

Post a Comment