Tuesday, February 7, 2017

DJIBRIL CISSE ATUNDIKA DALUGA.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa na Liverpool, Djibril Cisse amestaafu rasmi soka akiwa na umri wa miaka 35. Mara ya kwanza Cisse alitangaza kupumzika soka kwa muda Octoba mwaka 2015 kwasababu ya majeruhi ya nyonga lakini alikuwa na matumaini ya kurejea baada ya kufanyiwa upasuaji mwaka jana. Nyota huyo alikuwa akifanya mazoezi na klabu ya Auxerre ili aweze kuwa fiti lakini baada ya kushindwa kupata mkataba ameamua kutundika daluga zake rasmi baada ya kupita miaka 17 katika soka. Kwasasa Cisse amepanga kujishughulisha na masuala ya U-DJ, utayarishaji na uchambuzi. Cisse ambaye ameichezea Ufaransa mechi 41, alikaa Liverpool kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2004 kabla ya nchini kwake katika klabu ya Marseille. Cisse pia amewahi kuichezea Sunderland, Panathinaikos, Lazio, QPR, Kuban Krasnodar na Bastia.

No comments:

Post a Comment