Tuesday, February 7, 2017

DIOUF AWAPONDA NYOTA WA CAMEROON WALIKATAA KWENDA AFCON.

NGULI wa zamani wa soka wa kimataifa wa Senegal, El-Hadj Diouf amesema wachezaji nane wa Cameroon waliokataa mwito wa kuichezea timu yao ya taifa katika michuano ya Mataifa ya Afrika watajutia uamuzi huo maisha yao yote. Nyota kadhaa wa Cameroon akiwemo Joe Matip anayekipiga Liverpool, Eric Choupo-Moting na Allan Nyom wote wakicheza Schalke walikataa kuitumikia nchi yao kwa madai binafsi haswa suala la kuchelewa kwa posho zao. Akizungumza na BBC, Diouf amesema haelewi watu wanaoikataa nchi yao kwa siku zote mtu anayekataa kwao, hafahamu atapokwenda. Diouf aliendelea kudai kuwa wachezaji hao watakuja kujuta pindi watakapomaliza kucheza soka lao kwani watakakuwa hawana pa kwenda. Diouf amesema siku zote ni ngumu kuwa Muafrika kwani hata kama ukiwa kocha mzuri namna gani lakini hawataweza kukupa klabu kama Barcelona, Paris Saint-Germain, Liverpool au Manchester United uzifundishe.

No comments:

Post a Comment