Tuesday, February 7, 2017

TIOTE ATIMKIA CHINA.

TIMU ya Beijing Enterprise Group imetangaza kumsajili Chick Tiote kutoka klabu ya Newcastle United. Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast anamalizia miezi minne ya mwisho katika mkataba wake St.James Park na alikuwa akitegemewa kwenda kujiunga na klabu ya Shandong Luneng inayoshiriki Ligi Kuu ya China. Hata hivyo, mambo yamebadilika na sasa nyota huyo mwneye umri wa miaka 30 amesaini katika klabu hiyo ambayo inashiriki ligi daraja la pili. Beijing ilithibitisha ujio wa Tiote sambamba na wachezaji wengine wanne wapya waliowasajili kupitia mtandao rasmi wa Weibo mapema leo.Tiote alijiunga na Newcastle akitokea FC Twente mwaka 2010 kwa kitita cha paundi milioni 3.5.

No comments:

Post a Comment