Monday, February 6, 2017

MARTIAL AKANUSHA TETESI ZA KWENDA PSG.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Anthony Martial amekanusha taarifa kuwa hana furaha katika klabu hiyo. Nyota huyo ameshindwa kupata nafasi katika kikosi cha United toka waliposhinda mabao 4-0 katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Wigan Athletic mwishoni mwa mwezi uliopita, na kuzusha tetesi juu ya mustakabali wake. Taarifa zilizozagaa zimekuwa zikimuhusisha na tetesi za kwenda Paris Saint-Germain lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 amekanusha kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter. Martial alikanusha taarifa hizo na kudai kuwa hakuna ukweli wowote katika taarifa hizo kwani anafurahia maisha Old Trafford.

No comments:

Post a Comment