Wednesday, February 8, 2017

SUAREZ BADO ANA MATUMAINI KUCHEZA FAINALI KOMBE LA MFALME.

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Luis Suarez ana matumaini rufani itakayokatwa itaweza kumuokoa asikose mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili dhidi ya Atletico Madrid. Suarez aliifungia Barcelona bao katika mchezo ambao ulishuhudia wachezaji watatu wakipewa kadi nyekundu katika sare ya bao 1-1 jana iliyofanya Barcelona kufuzu fainali ya nne mfululizo kwa jumla ya mabao 3-2. Hata hivyo nyota huyo wa kimataifa wa Argentina litolewa nje kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu aliyokaa Barcelona baada ya mwamuzi kudhani alimpiga kiwiko Koke katika dakika za majeruhi. Akizungumza na wanahabari Suarez amesema kadi hiyo aliyopewa inamfanya ajisikie kucheka kwani inaonekana kama mwamuzi alidhamiria kufanya hivyo. Suarez aliendelea kudai kuwa wanataka kuona kama wanaweza kukata rufani kwasababu hadhani kama alifanya kosa lolote kustahili adhabu hiyo.

No comments:

Post a Comment