Wednesday, February 8, 2017

RAFEL NADAL ANATAKA URAIS REAL MADRID.

NYOTA wa tenisi na bingwa mara 14 wa mataji ya Grand Slam, Rafael Nadal raia wa Hispania amebainisha angependa siku moja kuwa rais wa Real Madrid. Ingawa mjomba wake Nadal, Miguel Angel Nadal alikuwa beki wa zamani wa Barcelona, yeye amekuwa tofauti kwani ni shabiki wa kutupwa wa Madrid. Nadal amekiri kuwa inaweza isiwezekane lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 amesema kuiongoza klabu hiyo ni moja ya ndoto zake. Madrid kwasasa wanaongoza La Liga wakitofautiana na Barcelona kwa alama nne huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi. Nadal ambaye alishindwa katika hatua ya fainali ya michuano ya wazi ya Australia mwezi uliopita, amepongeza kazi nzuri inayofanywa na rais wa sasa Florentino Perez.

No comments:

Post a Comment