Wednesday, February 8, 2017

LAHM KUTUNDIKA DARUGA MWISHONI MWA MSIMU.

NAHODHA wa Bayern Munich, Philipp Lahm anatarajiwa kustaafu rasmi soka mwishoni mwa msimu huu. Akiwa chini ya mkataba mpaka mwaka 2018, Lahm ametangaza mpango wake wa kustaafu mapema jana katika mchezo wa DFB-Pokal walishinda bao 1-0 dhidi ya Wolfsburg. Akiulizwa kuhusu mustakabali wake na wanahabari, Lahm alithibitisha kuwa atastaafu mwishoni mwa msimu. Bayern walikuwa wakitaka kumpa kibarua Lahm cha mkurugenzi mpya wa michezo msimu ujao lakini mwenye anadhani ni mapema sana kukubali kufanya kazi hiyo. Lahm ambaye kipindi chake chote cha soka ameitumikia Bayern, amefanikiwa kushinda mataji saba ya Bundesliga, sita ya DFB-Pokal, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Klabu Bingwa ya Dunia. Beki huyo wa pia alikuwa nahodha wa Ujerumani katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 wakati walipoitandika Argentina bao 1-0 katika mchezo wa fainali.

No comments:

Post a Comment