Wednesday, February 8, 2017

KOCHA WA ROMA AANZA JEURI BAADA YA KUICHAPA FIORENTINA.

KOCHA wa AS Roma, Luciano Spalletti anataka wachezaji wake kutumia ari ya Super Bowl ili kuweza kuwafikia vinara wa Serie A Juventus. Mabao mawili ya Edin Dzeko yaliisaidia Roma kuishindilia mabao 4-0 Fiorentina jana na kuwafanya kukwea mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa ligi. Roma wako alama nne nyuma ya mabingwa watetezi Juventus ambao wana mchezo mmoja mkononi. Lakini baada ya kuangalia New England Patriots wakitoka nyuma kwa alama 25 na kuitandika Atlanta Falcons kwa 34-28 katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mpira wa Miguu wa Kimarekani-NFL maarufu kama Super Bowl, Spalletti anaamini wataweza. Akizungumza na wanahabari, Spalletti amesema wamekuwa na msimu mzuri kama ilivyokuwa kwa Juventus na Napoli hivyo ni wajibu wao kuamini wanaweza mpaka mwisho.

No comments:

Post a Comment