BILIONEA mwanzilishi wa wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates na mmiliki wa timu ya New England Patriots, Robert Kraft wanadaiwa kuwahi kupewa nafasi ya kununua klabu ya Liverpool wakati Tom Hicks na George Gillett walipomaliza muda wao. Taarifa hizo zimebainika katika nyaraka za mahakama katika kesi ya kisheria inayoendelea kati ya kampuni inayoitwa Mill Financial, Gillett na Royal Bank ya Scotland. Hicks na Gillett walikubali kuiuza Liverpool Aprili mwaka 2010 wakati waliposhindwa kulipa fedha walizokopa kuinunua klabu hiyo mwaka 2007. Barclays Capital waliteuliwa kutafuta wanunuzi na nyaraka zilizoonyeshwa katika mahakama kuu huko New York zinaonyesha kuwa Gates alifuatwa wakati akitafutwa mtu atakayeweza kuinunua timu hiyo. Mwenyekiti wa wakati huo wa Liverpool Sir Martin Broughton, alipohojiwa kuhusiana na suala hilo alikiri kuwa ni kweli. Kampuni ya New England Sports Ventures inayojulikana kwasasa kama Fenway Sports Group ndio waliofanikiwa kuinunua Liverpool kwa kitita cha paundi milioni 300 Octoba mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment