Wednesday, February 8, 2017

MAJERUHI YAENDELEA KUITESA BARCELONA.

KLABU ya Barcelona imethibitisha kuwa beki wake Javier Mascherano amepata majeruhi ya mguu wa kushoto. Mascherano aliingia katika dakika ya 62 akitokea benchi kuchukua nafasi ya Denis Suarez wakati wa mchezo wa jana wa nusu fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Atletico Madrid. Beki huyo alikamilisha dakika zote za mchezo lakini alionekana kama akichechemea mara baada ya kipenga cha mwisho. Taarifa za kitabibu zilizotangazwa leo zimeonyesha kuwa beki huyo aliumia mguu na kurejea kwake uwanjani kutategemea kupona kwake. Pamoja na kwamba haujatolewa muda kamili wa kurejea uwanjani lakini inadaiwa kuwa anaweza kukaa nje kwa wiki mbili mpaka tatu hivyo kuwepo uwezekano wa kukosa mchezo wa Jumanne ijayo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain-PSG.

No comments:

Post a Comment