Wednesday, February 8, 2017

RAIS WA ATLETICO AIZODOA MAN UNITED KUHUSU GRIEZMANN.

RAIS wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo amepuuza tetesi kuwa Antoine Griezmann anatarajia kwenda kujiunga na Manchester United majira ya kiangazi, akisisitiza kuwa mshambuliaji huyo anafurahi kuwepo hapo. Wiki iliyopita zilizagaa taarifa kuwa United inamuwinda Griezmann na wako tayari kutoa kitita cha euro milioni 100, huku wengine wakienda mbali zaidi na kudai pande zote mbili zimeshaafikiana suala hilo. Hata hivyo, Griezmann yuko katika msimu wake wa tatu Atletico na ana mkataba unaomalizika Juni mwaka 2021 na Cerezo kuongeza kuwa nyota huyo ni bora na anafurahia maisha Atletico. Cerezo amesema ni vigumu kwa wachezaji wao kuondoka kwani wanafurahia maisha ya hapo na Griezmann bado ana mkataba nao.

No comments:

Post a Comment