Thursday, March 9, 2017

ARSENAL YAMTENGENGEA FUNGU NONO OZIL.

KIUNGO wa Arsenal, Mesut ozil anadaiwa kutengewa ofa nono ya mshahara unaofikia paundi 280,000 kwa wiki ili aweze kubakia katika klabu hiyo. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani bado hajaamua kuhusu muskabali wake huku ikiwa imebaki miezi 15 katika mkataba wake wa sasa, na kumekuwa na wasiwasi uliobuka kuwa anaweza kuondoka kiangazi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 tayari ndio mchezaji anayelipw zaidi Arsenal akikunja kitita cha paundi 140,000 kwa wiki ambazo zinaongezeka mpaka kufikia paundi 200,000 kwa wiki ukiongeza na bakshishi. Arsenal wako tayari kumuongeza zaidi lakini Ozil anaonekana kutokuwa tayari akifahamu kuwa anaweza kupata zaidi akienda kwingineko.

No comments:

Post a Comment