Thursday, March 9, 2017

L.A GALAXY WAMTEGA IBRAHIMOVIC.

KLABU ya Los Angeles Galaxy imemwambia Zlatan Ibrahimovic kuwa wanajiandaa kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya Soka ya Marekani-MLS kama akijiunga nao akitokea Manchester United majira ya kiangazi. Ibrahimovic alijiunga na United kwa mkatab wa mwaka mmoja kiangazi mwaka jana huku kukiwa na kipengele cha kuongezewa miezi mingine 12. Lakini wakati United wakitaka kumuongeza mkataba mwingine ili abakie Old Trafford nyota huyo mwenye umri wa miaka 35 bado hajakubali. Ibrahimovic ameifungia United mabao 26 msimu huu katika mashindano yote huku akitarajiwa kuanza katika mchezo wa Europa League mkondo wa kwanza hatua ya 16 bora dhidi ya Rostov ya Urusi baadae leo. Mwaka jana mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Kaka ndiye mchezaji aliyekuwa akilipwa fedha nyingi zaidi MLS, akikunja kitita cha dola milioni 7.167 kwa mwaka katika klabu ya Orlando City.

No comments:

Post a Comment