Thursday, March 9, 2017

WENGER AWAACHIA MASHABIKI KUAMUA HATMA YAKE.


MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema mawazo ya mashabiki yanaweza kuchangia uamuzi wake wa aidha abaki au aendelee kuifundisha klabu hiyo msimu ujao. Kundi la mashabiki wa Arsenal waliandamana baada ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya waliotandikwa mabao 5-1 na Bayern Munich katika Uwanja wa Emirates juzi. Akizungumza na wanabahri kuhusu suala la mustabali wake na mashabiki wa timu hiyo, Wenger amesema anatarajia suala hilo halitakuwa kitu muhimu lakini atalifikiria kabla ya kufanya uamuzi wake. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa amefanya kazi kwa bidii kwa miaka 20 ili kuwafurahisha mashabiki na wakati wanapopoteza anafahamu wanakosa furaha hiyo. Wenger amekuwa meneja wa Arsenal, toka Octoba mwaka 1996, na anatarajiwa kutangaza mwezi ujao kama atabaki aua kuondoka, lakini amekanusha taarifa kuwa tayari amehawaambia wachezaji wake uamuzi wake.

No comments:

Post a Comment