Thursday, March 9, 2017

ALONSO KUSTAAFU SOKA MWISHONI MWA MSIMU.

KIUNGO wa Bayern Munich, Xabi Alonso ametangaza nia yake ya kustaafu soka rasmi pindi msimu utakapomalizika majira ya kiangazi. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35, amecheza mechi 27 za Bayern msimu huu, ikiwemo kucheza dakika zote 180 katika ushindi wa jumla ya mabao 10-2 kweney hatua ya 16 bora dhidi ya Arsenal. Kulikua taarifa zilizozagaa mapema msimu huu kuwa Alonso anafikiria kutundika daruga zake huku Philipp Lahm pia naye akiushangaza ulimwengu kwa uamuzi wake lakini bado haijawa rasmi mpaka sasa. Alonso alituma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter mapema leo asubuhi akidai kuwa aliishi na kupenda kwaheri soka mchezo mzuri. Baada ya hapo aliiambia tovuti ya Bayern kuwa haikuwa uamuzi rahisi lakini anaamini ni wakati sahihi kwani siku zote amekuwa na akifikiri ni vyema kustaafu mapema. Alonso alianza soka lake Real Sociedad mwaka 1999 kabla ya kunaswa na Liverpool miaka minne baadae.

No comments:

Post a Comment