Thursday, March 9, 2017

RAIS WA PSG AKIRI KUTOAMINI KILICHOTOKEA.

RAIS wa Paris Saint-Germain-PSG, Nasser Al-Khelaifi amesema ni vigumu kukubali kutolewa kwao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia kupoteza wao dhidi ya Barcelona. PSG walitinga katika mchezo huo wakiwa mbele kwa mabao 4-0 waliyopata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika huko Parc des Princess lakini mambo yalibadilika na kushudia Barcelona wakiweka rekodi mpya ya kupindua matokeo hayo na kushinda mabao 6-1 jana katika Uwanja wa camp Nou. Barcelona walifunga mabao matatu kuanzia dakika ya 88 ikiwemo bao la ushindi la Sergi Roberto alilofunga mwishoni wa dakika tano za muda wa nyongeza. Akizungumza na wanahabari, Al-Khelaifi amesema pamoja na kuwa walistahili kupata paneti mbili lakini ukweli ni kwamba hawakucheza vizuri katika kipindi cha kwanza. Rais huyo alindelea kudai kuwa baada ya kushinda mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza ni vigumu kukubali kupoteza kwa mabao 6-1 lakini hawana jinsi kwani ndio imeshatokea.

No comments:

Post a Comment