Friday, March 10, 2017

HART AKATA TAMAA YA KUREJEA MAN CITY.

KIPA wa kimataifa wa Uingereza, Joe Hart amesema yeye ni hitaji la ziada kwa Manchester City na haoni kama ataweza kuitumikia klabu hiyo ya Ligi Kuu tena. Hart alijiunga kwa mkopo na Torino ya Italia kwa msimu mzima Agosti mwaka huu baada ya kuambiwa yuko huru kuondoka na meneja Pep Guardiola. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 aliongeza kuwa aliona uamuzi wa kumuacha katika kikosi cha meneja huyo unakuja ndio maana akaamua kuondoka. Akizungumza na wanahabari, Hart amesema kama unafahamu huwezi kushinda hakuna maana ya kupambana haswa kwa mtu mwenye nguvu kama yule. Hata hivyo, Hart aliendelea kudai kuwa anaamini uamuzi wa Guardiola haukuwa binafsi na anamheshimu kocha huyo.

No comments:

Post a Comment