Wednesday, March 1, 2017

JOE HART NJIA PANDA CITY.

MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola anatarajiwa kutofanya uamuzi wowote kuhusu mustakabali wa Joe Hart mpaka itakapofika mwishoni mwa msimu. Inategemewa kuwa kipa huyo wa kimataifa wa Uingereza anaweza kuondoka City moja kwa moja wakati mkopo wake katika klabu ya Torino utakapomalizika Mei mwaka huu. Nyota huyo mwneye umri wa miaka 29 ameripotiwa kuzivutia klabu kadhaa za Uingereza na Ulaya. Akiulizwa na wanahabari kuhusu Hart, Guardiola ambaye anafurahia kuwa makipa Willy Caballero na Claudio Bravo amesema suala hilo atalizungumzia msimu utakapomalizika. Bravo amekuwa akikosolewa toka atue Etihad akitokea Barcelona kwa kitita cha paundi milioni 15.4 Agosti mwaka jana.

No comments:

Post a Comment