Wednesday, March 1, 2017

CHINA YAIZIDI UINGEREZA KATIKA USAJILI.

KLABU za China zimetumia kitita cha paundi milioni 331 wakati wa usajili wa majira baridi, kiasi ambacho kimepita kile kilichotumiwa na klabu za Ligi Kuu Uingereza. Dirisha la usajili nchini humo lilifungwa Jumanne iliyopita, huku klabu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya China zikipita kiasi cha paundi milioni 215 zilizotumiwa na klabu 20 za Ligi Kuu Uingereza. Uhamisho wa Oscar kutoka Chelsea kwenda Shanghai SIPG uliogharimu paundi milioni 60 na ule wa Carlos Tevez kutoka Boca Juniors kwenda Shanghai Shenhua kwa kitita cha paundi milioni 40, ndio uliogharimu kiasi kikubwa cha fedha. Msimu mpya wa ligi nchini humo unatarajiwa kuanza na sheria mpya ambayo inazuia idadi ya wachezaji wageni wanaotumika. Wachezaji watatu pekee wa kigeni ndio wanaweza kuruhusiwa kucheza katika mechi moja wakati msimu utakapoanza mwezi huu.

No comments:

Post a Comment