Wednesday, March 1, 2017

LEICESTER WAFANYA MAZUNGUMZO NA HODSON KUHUSU NAFASI YA RANIERI.

MABINGWA wa Ligi Kuu Leicester City wamefanya mazungumzo rasmi na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodson kuhusu kuwa meneja mpya wa klabu hiyo. Hata hivyo, taarifa zinadai kuwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 69 ndiye pekee Leicester waliyezungumza naye katika kutafuta mbadala wa Claudio Ranieri. Meneja wa muda wa Leicester Graig Shakespeare anaweza kuendelea kuinoa klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu kama akiendelea kupaa matokeo mazuri. Ranieri alitimuliwa Februari 23 mwaka huu, miezi tisa baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment