Thursday, March 2, 2017

PODOLSKI KUKIMBILIA JAPAN.

MSHAMBULIAJI wa Galatasaray, Lukas Podolski ametangaza kuondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu na kwenda klabu ya Vissel Kobe ya inayoshiriki J League ya Japan. Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani na mshindi wa Kombe la Dunia bado alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja katika klabu hiyo Uturuki. Podolski anadaiwa kutafuta changamoto mpya baada ya kucheza kwa miaka mingi na mafanikio barani barani Ulaya. Podolski alijiunga na Galatasaray akitokea Arsenal kiangazi mwaka 2015, akiwa pia amewahi kucheza katika klabu za Koln na Bayern Munich zote za Ujerumani.

No comments:

Post a Comment