Thursday, March 2, 2017

WENGER AKANUSHA TETESI ZA BARCELONA.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amejiweka pembeni kufuatia taarifa zinazodai kuwa anaweza kuwa mshindani katika harakati za kuziba nafasi ya Luis Enrique katika klabu ya Barcelona. Nafasi ya kocha kwa klabu hiyo itakuwa wazi majira ya kiangazi kufuatia Enrique kutangaza kuwa ataachia ngazi msimu ukimalizika. Kufuatia tetesi za kuondoka Arsenal huku mkataba wake ukiwa nao ukiwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu bila kuwepo dalili za kuongeza, Wenger amekuwa akihusishwa nafasi hiyo ya kwenda Camp Nou. Hata hivyo akihojiwa kuhusiana na suala hilo, Wenger amesema kwasasa hatafuti kibarua kwani bado ana majukumu Arsenal. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa jambo muhimu analofanya hivi sasa ni kuhakikisha anairejesha Arsenal katika makali yake ili wamalize msimu wakiwa juu.

No comments:

Post a Comment