Thursday, March 2, 2017

BOLIVIA YAKATA RUFANI CAS.

BOLIVIA imekata rufani Mahakama ya Michezo ya Kimataifa-CAS baada ya kukatwa alama nne katika mechi zake za kufuzu Kombe la Dunia kwa kosa la kuchezesha mchezaji asiyestahiki. Bolivia iliichapa Peru mabao 2-0 nyumbani na baadae kutoka sare ya bila kufungana na Chile ugenini katika wiki ya kwnza ya Septemba, lakini kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ilitoa ushindi wa mabao 3-0 kwa timu hizo mbili walizocheza nazo. FIFA iliilima adhabu hiyo Bolivia kwa kumchezesha Nelson Cabrera mzaliwa wa Paraguay wakati alikuwa hastahili kucheza. Bolivia tayari walishapoteza rufani yao waliyokata FIFA. Hatua hiyo hiyo iliathiri kwa kiasi kikubwa msimamo wa kundi kwa nchi za Amerika Kusini ambapo timu nne kati ya 10 zilizopo ndio zitafuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 huko nchini Urusi. Kundi hilo linaongozwa na Brazil wenye alama 27, wakifuatiwa na Uruguay wenye alama 23, Ecuador na Chile wote wana alama 20 wakishika nafasi ya tatu na nne wakati Argentina wako nafasi ya tano wakiwa na alama 19 na Colombia nafasi ya sita wakiwa na alama 18.

No comments:

Post a Comment