Thursday, March 2, 2017

OZIL FITI KUIVAA LIVERPOOL JUMAMOSI.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema Mesut Ozil atakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Liverpool pamoja na kuumwa, wakati Aaron Ramsey na Laurent Koscielny nao watakuwepo baada ya kupona majeruhi yaliyokuw ayakiwasumbua. Ozil alikosa mazoezi ya Arsenal mapema leo baada ya kutojisikia vyema lakini Wenger amedokeza kuwa anategemea kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani atakuwepo katika mchezo huo utakaofanyika Anfield keshokutwa. Pia Arsenal ilipata ahueni kufuatia nyota wake majeruhi Ramsey na Koscielny kurejea mazoezini mapema wiki hii, na Wenger amethibitisha kuwa wote wako fiti kwa ajili ya mchezo huo. Ramsey hajachza toka Januari kutokana na majeruhi ya kigimbi, wakati Koscielny yeey alitolewa nje kutokana na majeruhi ya msuli wa paja katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya waliyofungwa mabao 5-1 na Bayern Munich. Hata hivyo, kiungo Santi Cazorla na Mohamed Elneny bado wanaendelea kujiuguza majeruhi.

No comments:

Post a Comment